KIMENUKA LANGO LA HORMUZ: Iran Yadai Kupiga na Kukimbiza Meli ya Kivita na Meli ya Kubeba Ndege ya Marekani!

 

Kulingana na ripoti ya Crossword News, mzozo mkali katika maji yanayozunguka Mfereji wa Hormuz umefungua ukurasa mwingine wa hatari katika mgogoro unaoendelea kati ya Iran na Marekani. Hii ni baada ya Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC) kudai kuwa makombora yake yamepiga meli kubwa ya kubeba ndege za kivita (aircraft carrier) pamoja na meli ya kivita ya Marekani (US Navy destroyer).

Ushuhuda huo kutoka Iran uliteka hisia za wengi mara moja kwa sababu ulionyesha tukio zito zaidi kuliko majibizano ya kawaida ya maonyo au urushaji wa makombora usiofanikiwa.

Iran ilidai kuwa meli hizo za kivita za Marekani zilipata uharibifu na kulazimika kukimbia na kuondoka katika eneo hilo. Hata hivyo, Serikali ya Marekani imetoa maelezo tofauti kabisa, ikisema kuwa makombora hayo ya Iran yalisambaratishwa kabla hayajapiga meli hizo na kwamba hakuna askari yeyote wa Marekani aliyejeruhiwa. Mvutano huu wa kauli unabaki kuwa jambo kuu la kufuatiliwa.

Jambo lililothibitishwa ni kwamba Iran ilirusha makombora kuelekea kwenye meli za kivita za Marekani zilizopo kwenye maji ya eneo hilo, na kufuatiwa na hatua ya Marekani kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya meli za mafuta za Iran.

Jeshi la IRGC lilisema kikosi chake cha anga kilirusha makombora kadhaa dhidi ya meli hizo za Marekani, zikiwatuhumu askari hao kwa kughasi vyombo vya usafiri wa baharini na kushiriki katika mpango wa Marekani wa kuweka presha ya kijeshi dhidi ya Iran.

Jeshi hilo lilidai kuwa baada ya meli hizo kupata uharibifu na kuogopa mashambulizi mengine ya kisasi, zililazimika kukimbia eneo la mapigano.

Kauli hiyo ilikuwa ni jaribio la Iran kuonyesha kuwa operesheni hiyo haikuwa tu jaribio la shambulio, bali ni ushahidi kwamba Iran ina uwezo wa kuzilazimisha zana kubwa za kijeshi za Marekani kubadili mwelekeo zikiwa karibu na pwani ya Iran.

Post a Comment

Previous Post Next Post