Kuongezeka kwa Mvutano Usiku Kucha: Marekani Yaishambulia Iran Wakati Tehran Ikirusha Makombora na Drones Kwenye Kambi za Kikanda.

Vikosi vya Marekani vilifanya mfululizo wa mashambulizi usiku kucha dhidi ya ngome za kijeshi za Iran kuzunguka Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa mujibu wa ripoti.


Meli za kivita (destroyers) aina ya Arleigh Burke-class zinaripotiwa kufyatua makombora ya BGM-109 Tomahawk kulenga maeneo kwenye Kisiwa cha Qeshm, pamoja na maeneo mengine huko Bandar Abbas, Bushehr, Sistan na Baluchestan.


Wakati huo huo, ndege za kivita za F/A-18F Super Hornet na F-35C zinaripotiwa kufanya mashambulizi kadhaa ya anga katika Jimbo la Hormozgan, zikilenga minara ya mawasiliano na intaneti, miundombinu ya umeme, mitambo ya makombora, na mifumo ya rada za pwani inayotumiwa kufuatilia mienendo ya meli baharini.


Majeshi ya Iran baadaye yalijibu mapigo kwa wimbi la makombora ya masafa marefu (ballistic missiles) na ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga (one-way drones) zikilenga Kambi ya Anga ya Muwaffaq Al-Salti na vituo vya kijeshi huko Aqaba, nchini Jordan.


Iran inaripotiwa kutumia kati ya makombora 13 hadi 14 ya masafa ya kati aina ya Kheibar Shekan, pamoja na drones aina ya Shahed-136 na Arash-2.


Mashambulizi ya ziada ya drones za Iran yanaripotiwa kulenga vituo vya kijeshi nchini Bahrain, ikiwemo Kambi ya Anga ya Sheikh Isa iliyopo karibu na mji mkuu Manama.


Majeshi ya Iran pia yalidai kudungua drone ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper iliyokuwa ikipaa kwenye anga ya Khomein.


Ripoti hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru, na taarifa rasmi kuhusu ukubwa kamili wa mashambulizi hayo, uharibifu uliotokea, na idadi ya majeruhi au vifo bado ni finyu. Mashambulizi haya ya hivi punde yanaashiria kupanda kwa kiwango kikubwa kwa mvutano unaopanuka kwa kasi kati ya Marekani na Iran.


Mashambulizi ya Marekani kulenga rada za pwani, minara ya mawasiliano, na miundombinu ya umeme katika Jimbo la Hormozgan ni mbinu ya kiasili ya kijeshi ya kumpofusha na kumfanya adui awe kiziwi.

 Marekani inajaribu kuondoa uwezo wa Iran wa kuona meli zinazopita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz na kuharibu uwezo wao wa kuratibu mashambulizi mapya.


Kujibu mapigo kwa Iran kwa kupiga kambi za Jordan (Aqaba) na Bahrain kunabadilisha sura ya mzozo huu. Sasa siyo tena Marekani na Iran pekee wanaoumia; washirika wa Marekani katika Mashariki ya Kati wameingizwa moja kwa moja kwenye uwanja wa vita. Hili linaweza kuzipa nchi hizo hofu na shinikizo kubwa la kisiasa ndani ya nchi zao.


Tofauti na miaka ya nyuma ambapo vita hivi vilipiganwa kupitia vikundi vya wanamgambo (proxies) kule Syria au Iraq, sasa ni vyuma vinagongana moja kwa moja. Marekani imepiga ndani ya ardhi ya Iran (Qeshm, Bandar Abbas), na Iran imerusha silaha zake nzito (Kheibar Shekan ballistic missiles) kulenga kambi rasmi za Marekani.

@Swahili Prime Media

Post a Comment

Previous Post Next Post