Juzi Iran ilishambulia meli mbili za kivita za Jeshi la Maji la Marekani. Nilishangaa sana kuona Marekani haikujibu mapigo. Lakini leo Marekani imeshambulia meli tatu za mafuta za Iran. Yaani, imeshambulia meli zinazobeba mafuta.
Hiyo inamaanisha Marekani imejaribu kulipiza kisasi kwa shambulio la Iran. Hapo nyuma, Marekani ilikuwa ikishambulia, kisha Iran inalipiza kisasi. Sasa Iran inashambulia, na Marekani inajaribu kulipiza kisasi. Hali ya Trump dhidi ya Iran imekuwa mbaya kiasi kwamba juzi waandishi wa habari walimuuliza:
Ni nchi gani inaleta tishio kubwa zaidi kwa biashara ya Marekani?
Unajua Trump alijibu nini? Alisema:
Canada ndiyo tishio kubwa zaidi kwa biashara ya Marekani.
Hakutaja China. Hakutaja Urusi. Hakutaja nchi nyingine yoyote. Aliitaja Canada—mshirika wa karibu zaidi wa Marekani! Profesa wa Marekani Richard Wolff alisema kwenye kipindi cha profesa wa Norway Glenn Diesen:
Hii ni hatua mpya ya ubeberu wa Marekani.
Alimaanisha kwamba dola ya Marekani sasa ipo kwenye njia ya kuporomoka. Hivyo itajaribu kutumia ushawishi wake kwa namna yoyote iwezavyo.
Profesa Wolff alisema Trump anaweza hata kuitangaza Canada kama jimbo la 51 la Marekani! Kama ambavyo siku chache zilizopita, alipost ramani ya Mlango-Bahari wa Hormuz kwenye mitandao yake ya kijamii, akidai kuwa ni mali ya Marekani!
Alidai hata Ziwa Ontario la Canada ni la Marekani! Sasa swali ni kwa nini anafanya hivi?
Mchambuzi wa kijiopolitiki na mwanauchumi wa Marekani Jeffrey Sachs alisema:
Mfuomo wa dunia uliojengwa kwenye uongo sasa unaporomoka.
Alimaanisha kwamba mfumo wa dunia ulioibuka baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, hasa baada ya Umoja wa Kisovieti kusambaratika mwaka 1991, chini ya uongozi wa Marekani—kiuhalisia ulijengwa kwenye uongo. Sitaingia kwenye mjadala wa kina. Ni jambo gumu. Ninalirahisisha ili kila mtu aelewe. Ngoja nitoe mfano mdogo tu.
Kabla ya Marekani, ni nchi gani tunazozifikiria kama nguvu za kibeberu? Uingereza, Ubelgiji, Uholanzi, Ufaransa, hizi nchi, sivyo?
Uingereza ilipata kuwa Uingereza ya leo kwa kupora utajiri wa bara dogo la India. Ubelgiji ikawa Ubelgiji ya leo kwa kupora rasilimali za Congo. Uholanzi ikawa Uholanzi ya leo kwa kupora rasilimali za Indonesia.
Kwa hiyo nchi za kibeberu zilitajirika na kuimarisha chumi zao hasa kwa kupora rasilimali za nchi nyingine. Mfumo wa dunia ulioanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili, chini ya mwavuli wa demokrasia na haki za binadamu, kiuhalisia ulikuwa umesimama kwenye uongo. Unajua kwa nini?
Profesa Michael Klare alisema:
Marekani ilikuwa inafanya kitu kile kile lakini kwa njia tofauti.
Iliingia Afghanistan kupora rasilimali, ikaingia Iraq, na hivi karibuni ikaingia Venezuela pia. Lakini ilisemaje ilipokuwa inaenda kwenye hizi nchi?
Ilizungumzia demokrasia na haki za binadamu. Kama vile ilivyotokea kwa Iran. Hakuna demokrasia Iran, hakuna haki za binadamu wakisema haya yote, wakaingia Iran pia. Lakini hawakujua kwamba Wairan hawako kama wengine. Wana ustaarabu wa maelfu ya miaka. Wako mbali sana kimaarifa na kisayansi. Hivyo wamekwama wakijaribu kupora rasilimali za Iran. Iran inawafundisha somo kila kukicha.
Lakini hali ya kiuchumi ya Marekani kwa sasa ni mbaya sana. Hivyo watafanya nini sasa? Wakati mwingine watataka kuichukua Canada. Wakati mwingine Greenland.
Dola zinapoporomoka, zinaanza kutenda hivi. Chukulia Puerto Rico, kwa mfano. Marekani imeikalia. Watu wake hawawezi kupiga kura kwenye chaguzi za rais wa Marekani. Lakini Marekani hiyo hiyo inaipa dunia darasa kuhusu demokrasia!
Leo Trump alitangaza:
Tutaenda kushambulia Mlima Pickaxe hivi karibuni.
Kusikia hivi, profesa wa Marekani Mearsheimer aliuliza:
Kwani Trump hakusema miezi mitatu iliyopita kwamba angeuharibu huu mlima?
Kwa hiyo hii itaendelea kwa miaka kadhaa zaidi. Baada ya kushindwa Iran, Marekani ya kibeberu itaenda kwenye nchi mbalimbali na kujaribu kupora rasilimali zao. Lakini itaendelea kushindwa katika maeneo mengi. Hiki ndicho Profesa Wolff anachokiita:
Hatua mpya ya ubeberu wa Marekani.
Hatua hii mpya si chochote bali ni mwanzo wa mwisho wa ubeberu wa Marekani. Mwaka 1991, utawala wa dola ya Marekani ulianza kwa kishindo na Iraq. Na anguko la dola hiyo hiyo limeanza na Iran.
@Swahili Prime Media
