Serikali ya Iran imesema marubani wake watatu wa Jeshi wameuawa wakati wa mashambulizi mapya ya Marekani yaliyolenga maeneo ya kusini mwa Iran.
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa marubani hao ni miongoni mwa wanajeshi waliopoteza maisha mapema wiki hii. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Iran, takriban watu 18 wameuawa na wengine 142 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Marekani yaliyofanywa kati ya Agosti 30 na Septemba 2.
Wakati mamlaka za Iran zikieleza kuwa maeneo kadhaa yameathiriwa, Marekani inasisitiza kuwa operesheni zake zililenga tu kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Iran (military capabilities).
Takwimu hizi za vifo na majeruhi zimetolewa na mamlaka za Iran na bado hazijathibitishwa na vyanzo huru vya kimataifa.
Kupoteza ndege ya kivita ni hasara ya kifedha, lakini kupoteza rubani wa jeshi ni hasara kubwa zaidi. Inachukua mamilioni ya dola na miaka mingi sana ya mafunzo kumtengeneza rubani mmoja wa kivita. Kifo cha marubani hawa watatu kinalipa jeshi la Iran pigo kubwa kwenye uwezo wao wa mashambulizi ya anga.
Kuwa na majeruhi 142 na vifo 18 kunaiweka serikali ya Iran chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi wake. Hii inawapa viongozi wa kijeshi uhalali wa kutekeleza kile walichokiita Shambulizi la Kiasimetria (kama kulenga Meli za Marekani) ili kutuliza hasira za wananchi.
@Swahili Prime Media