Nani Ana Jeshi Imara Zaidi Kati ya Marekani na Iran? (Ulinganisho wa 2026)


Mvutano kati ya Marekani na Iran umekuwa ukifukuta kwa miongo kadhaa, lakini matukio ya hivi karibuni Mashariki ya Kati yameifanya dunia ijiulize swali moja gumu: Je, kama vita vya moja kwa moja vikizuka leo kati ya mataifa haya mawili, nani ataibuka mshindi?

Kwenye makala hii, tunachambua uwezo wa kijeshi wa Marekani na Iran katika maeneo manne makuu ili kupata picha halisi ya nani ana ubabe wa kivita mwaka huu.

1. Bajeti ya Kijeshi na Nguvu ya Kiuchumi

Tukianza na mzunguko wa pesa, Marekani ni mbuyu ambao haulinganishwi na taifa lolote duniani. 

 ■Marekani: Inatumia zaidi ya Dola Bilioni 800 kila mwaka kwenye jeshi lake. Hii inawapa uwezo wa kutengeneza silaha za kisasa zaidi, kulipa wanajeshi vizuri, na kuweka kambi kila kona ya dunia.

 ■Iran: Kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyodumu kwa miaka mingi, bajeti ya jeshi la Iran ni chini ya Dola Bilioni 10. 

2. Jeshi la Anga na Teknolojia

Kwenye anga, mambo yako hivi:

 ■Marekani: Inaongoza dunia kwa kuwa na ndege za kivita za kisasa zaidi (5th Generation) kama F-35 na F-22 Raptor, ambazo haziwezi kuonekana kwenye rada (Stealth). Marekani inaweza kushambulia eneo lolote duniani ndani ya saa chache.

 ■Iran: Ndege nyingi za kivita za Iran ni za zamani (kama F-14 Tomcat walizonunua miaka ya 1970). Hata hivyo, Iran wamebuni mbinu mbadala; wamewekeza nguvu kubwa kwenye Teknolojia ya Drones (kama Shahed) na Makombora ya Masafa Marefu (Ballistic Missiles) ambayo yanaweza kufika kambi yoyote ya Marekani Mashariki ya Kati.

Marekani ina tawala anga, lakini makombora na ndege nyuki (Drones) za Iran ni tishio kubwa linalotisha mifumo ya ulinzi ya Marekani.

3. Jeshi la Majini (Navy) na Lango la Hormuz

■Marekani: Ina meli kubwa za kubeba ndege za kivita (Aircraft Carriers) zinazotembea kama miji inayoelea baharini. Zinaweza kusogea karibu na nchi yoyote na kuanza mashambulizi mazito.

■Iran: Iran haina meli kubwa kama za Marekani. Lakini wamewekeza kwenye Vita Vya Kushtukiza (Asymmetric Warfare). Wana maelfu ya boti ndogo zenye mwendo kasi zilizofungwa makombora, na nyambizi (submarines). Zaidi ya yote, Iran inadhibiti Lango la Hormuz, njia kuu ya mafuta duniani. Wakifunga lango hili, uchumi wa dunia unashuka.

Marekani ina nguvu kubwa baharini, lakini kijiografia, Iran ina faida ya uwanja wa nyumbani.

4. Washirika na Vikundi Ndani ya Mkoa (Proxies)

■Marekani: Inaungwa mkono na nchi za Ulaya (NATO), Israel, na baadhi ya mataifa ya Kiarabu yenye nguvu za kiuchumi.

■Iran: Badala ya kutegemea majeshi ya nchi nyingine, Iran imeunda mtandao hatari sana unaoitwa Axis of Resistance (Mhimili wa Upinzani). Hili ni kundi la wanamgambo wenye silaha nzito akiwemo Hezbollah (Lebanon), Houthis (Yemen), na makundi ya Iraq na Syria. Iran inaweza kuitumia Marekani vita katika nchi nne tofauti kwa wakati mmoja bila hata kutuma mwanajeshi mmoja wa Iran.

Kwenye Vita vya Kawaida (Conventional Warfare) vinavyopiganwa uso kwa uso, Marekani itashinda kwa sababu ya nguvu kubwa ya teknolojia na bajeti. 

Lakini, Iran inajua haipaswi kupigana uso kwa uso. Kupitia makombora yao, drones, na vikundi vya wanamgambo, Iran imetengeneza mazingira ambayo yataifanya Marekani ipoteze mabilioni ya dola na maisha ya wanajeshi wengi ikiwa itajaribu kuivamia. Ni vita ambayo Marekani inaweza kushinda, lakini kwa hasara kubwa ambayo hawapo tayari kuipata.

Post a Comment

Previous Post Next Post