MWIKO WAVUNJWA BAADA YA MIAKA 80: Jinsi Iran Ilivyolazimisha Manowari ya Marekani Kukimbia Makombora Ghubani, Pentagon Yachanganyikiwa!


Katika miaka themanini tangu shambulio la Pearl Harbor, hakuna aliyethubutu kuigusa manowari ya Marekani ya kubeba ndege za kivita (Aircraft Carrier). Sasa, Iran imefanya jambo hilo haswa. Ripoti ya shirika la habari la BBC inasema:

Manowari ya Marekani ya kubeba ndege na ile ya kuharibu makombora zilifanikiwa kukwepa mashambulizi kadhaa.

Ni kukwepa tu (evaded). Sio kuharibu, sio kutungua. Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) yenyewe imekiri kwamba manowari ya USS George Washington ilibidi ifanye mbinu za kukwepa chini ya mvua ya makombora ya Iran. Manowari inayoendeshwa kwa kawi ya nyuklia ya jeshi lenye nguvu zaidi duniani ilibidi ipishe njia.


Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilifyatua makombora ya balestiki kuelekea kwenye manowari hiyo na meli nyingine ya ulinzi. Iran inadai meli zote mbili ziliharibiwa na kulazimishwa kuondoka eneo la mapambano. CENTCOM inasema hakuna meli iliyopigwa. (Hadi sasa bado hakuna uthibitisho huru wa madai ya Iran


Sasa swali ni: Je, Iran inaweza kweli kuzamisha manowari ya Marekani?

Aliyekuwa afisa wa ujasusi wa Marekani, Malcolm Nance, alipinga madai ya Iran kwa hoja thabiti ya kiufundi.mamia ya mitambo ya kutungua makombora hufanya kazi kulinda manowari, na lile jengo kubwa la chuma halizamishwi na makombora matatu au manne. Kuizamisha, lazima utoboe upande wake wa chini chini ya maji.

Hapa nakubaliana kwa kiasi fulani na Nance. Kiufundi yuko sahihi. Lakini kuzamisha haijawahi kuwa lengo la Iran. Ukiifanya manowari ishindwe kufanya kazi (non-operational), inakaa nje ya huduma kwa miaka kadhaa. Na kisiasa, picha ya manowari ya Marekani ikiungua katika Lango la Hormuz ina thamani kubwa kuliko uharibifu wa kifizikia.

Danny Citrinowicz, mchambuzi wa masuala ya Iran katika Taasisi ya Mafunzo ya Usalama wa Taifa ya Israel, amelenga ndipo. Kwa mtazamo wake, kitendo chenyewe cha kuilenga manowari kinathibitisha kuwa sasa Tehran iko tayari kuchukua tahadhari/hatari ambayo zamani ilikwepa makusudi. Nakubaliana naye. Iran imeacha kujali kuhusu madhara.


Kisasi cha Marekani na Uhalifu wa Kivita

Ndani ya saa chache, Marekani ilijibu. CENTCOM ilisema meli mbili za mafuta za Iran zimelemazwa kabisa na ya tatu imeharibiwa kabisa katika Ghuba ya Oman. Jeshi la Wanamaji la IRGC nalo likadai kushambulia meli kadhaa za mafuta na droni ya majini ya Marekani.

Sasa tuje kwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth. Alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba ikiwa Iran itashambulia meli za Marekani, Marekani itazamisha meli za mafuta za Iran. Alielezea kundi la meli za Iran kama zisizo na ulinzi (defenceless). Kwa maneno ya Kamanda wa CENTCOM, Admeli Brad Cooper, ukishambulia meli mbili, tatu zitachukuliwa kama kisasi. 

Kitu kimoja kinapaswa kusemwa wazi hapa. Kutambua hadharani meli za kiraia za kibiashara zisizo na ulinzi kama shabaha rahisi, kutangaza hivyo, na kisha kuzishambulia kunaingia kwenye tafsiri ya uhalifu wa kivita. Wizara ya mambo ya nje ya Iran imeiita hatua hiyo ukiukwaji wa wazi wa Ibara ya 2(4) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.


Hali ya Sintofahamu Ndani ya Washington.

Sasa sikia kinachoendelea ndani ya Washington. Uchunguzi wa New York Times unaripoti kuwa mwezi Agosti takriban maafisa 50 wa Kamandi ya Pamoja walilazimishwa kufanyiwa vipimo vya kutambua uongo. Swali lilikuwa moja tu — je, wao ndio waliovujisha habari kwamba akiba ya silaha za Marekani kwa ajili ya vita dhidi ya Iran inakaribia kuisha? Kituo cha CBS kinasema makumi ya maafisa wa CENTCOM walifanyiwa kipimo hicho hicho. Msemaji wa Pentagon, Sean Parnell, alisema hawatoi maoni kuhusu uchunguzi wa ndani.

Hivi sivyo upande unaoshinda unavyotenda. Utawala unaodai unashinda vita hauwafungi maafisa wake kwenye mashine ya kupima uongo. Hegseth amekanusha ripoti hizo za uhaba, na Trump ameiita habari zinazokosoa vita hivyo kuwa ni uhaini.

Tazama pia maoni ya umma. Kura za maoni za hivi punde za Reuters/Ipsos zinaonyesha kiwango cha kukubalika kwa Trump kimekwama asilimia 33, kiwango cha chini zaidi katika mihula yake yote miwili. Katika kura ya maoni ya Chuo Kikuu cha Massachusetts Amherst, asilimia 80 ya Wamarekani wanatarajia vita vya muda mrefu, na uungwaji mkono wa hatua za kijeshi nchini Iran umeshuka hadi asilimia 31.


Lengo Kuu: Nani Anadhibiti Mkondo wa Maji?

Maneno muhimu zaidi ya siku yalitoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa CIA na kamanda wa zamani wa CENTCOM, Jenerali David Petraeus. Alikubali kuwa mashambulizi yameharibu vibaya uwezo wa kijeshi wa Iran sehemu kubwa ya jeshi la majini imezamishwa, na kikosi cha anga hakipo tena. 

Lakini kisha akauliza swali la msingi: Je, Iran inaweza kutoka kwenye hili ikiwa dhaifu kijeshi lakini imara zaidi kistratijia? Jibu lake — hilo linategemea kabisa nani atamaliza akiwa anadhibiti Lango la Hormuz.


Kutokana na ukiri huu wa mkurugenzi wa zamani wa CIA, unaweza kujua Marekani imesimama wapi. Trump alianza vita kubadili serikali na sasa amekwama kwenye vita vya kugombea mkondo wa maji. Hili halitamalizwa kwa kuhesabu makombora. Yeyote anayedhibiti mtiririko wa mafuta na gesi ndiye mshindi. Na madai ya kudhibiti hayaendani na ukweli. Mwezi uliopita Trump alisema lango hilo liko chini ya udhibiti kamili wa Marekani. Lakini kwa hesabu za Kpler, wastani wa meli 13 tu kwa siku sasa ndizo zinazopita Hormuz.

Bungeni siku ya Jumapili, Spika wa Iran Mohammad Baqer Qalibaf alisema enzi za kujibu mashambulizi kulingana na kiasi cha uchokozi (proportionate response) zimekwisha. Pigo lolote dhidi ya maslahi ya Iran sasa litajibiwa kwa haraka, kwa uzito zaidi na kwa maumivu zaidi. Tazama zamani  baada ya Soleimani kuuawa, Iran ilirusha makombora machache kwenye kambi za Iraq na kuishia hapo. Qalibaf anasema siku hizo zimepita. Kwa kufyatulia makombora manowari, Iran tayari imeonyesha inamaanisha.


Msemaji wa IRGC, Hossein Mohebi, alisema siku hiyo hiyo kuwa kwa kila dola ya uharibifu ambayo Marekani inaisababishia Iran, inajisababishia yenyewe mara kadhaa zaidi. Hiyo ndiyo doktrini ya Tehran  sio ushindi wa kijeshi, bali kutokwa na damu kiuchumi.

Mwisho, neno kuhusu watu wa kawaida. Makombora ya kujihami yanayotumika juu ya Hormuz ni yale yale ambayo Ukraine haina tena kulinda gridi yake ya umeme. Vita moja inakula nyigine, na mshtuko wa bei za mafuta unatua kwenye mifuko ya ununuzi kutoka Asia Kusini hadi Afrika. 

Kwa miaka themanini hakuna aliyethubutu kuitazama manowari hiyo usoni. Wiki hii ilibidi isogee. Nani kazamisha nini sio hoja. Hoja ni kwamba woga umevunjika.

Endelea Kuifuatilia Swahili Prime Media kwa habari zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post