Gazeti la The Wall Street Journal linaripoti kwamba mashirika ya China yanadaiwa kuipatia Iran picha za setilaiti zenye ubora wa hali ya juu kabla ya shambulio la Iran la Julai 17 dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani ya Muwaffaq Salti nchini Jordan.
Wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Maafisa wa Marekani wanaripotiwa kushuku kuwa picha hizo huenda ziliisaidia Tehran kutambua vyema na kupata maeneo hasa iliyoyalenga. Hata hivyo, uhusika halisi wa wasambazaji hao wa China bado haujulikani wazi, na hakuna ushahidi uliothibitishwa wa ushiriki wa moja kwa moja wa serikali ya China katika shambulio hilo.
Taarifa hii kutoka Wall Street Journal inaingia ndani zaidi kwenye mzizi wa mgogoro wa kisasa. Hili sio tu suala la makombora kurushwa; ni suala la nani anamiliki taarifa za uwanja wa vita.
Kambi ya Muwaffaq Salti iliyopo Jordan sio kambi ya kawaida. Ni moja ya vituo muhimu sana vya kimkakati kwa Jeshi la Anga la Marekani katika Mashariki ya Kati, ikitumika kwa operesheni za ndege zisizo na rubani (drones) na ndege za kivita. Kwa Iran kufanikiwa kupiga kambi yenye ulinzi mkali kiasi hiki na kusababisha maafa, inamaanisha walikuwa na ramani kamili na sahihi ya wapi majengo ya kulala wanajeshi yalipo. Hapa ndipo picha za setilaiti zinapoingia.
Siri ya Kutumia Mashirika Badala ya Serikali (Plausible Deniability):
Mashirika ya China (Chinese entities) na hakuna ushahidi wa serikali ya China kuhusika moja kwa moja. Kwenye siasa za kimataifa, hii inaitwa Plausible Deniability (uwezo wa serikali kukanusha kwa mantiki). Nchi kubwa zinaweza kutumia makampuni binafsi kuuza silaha au taarifa za kijasusi kwa nchi washirika kama Iran. Hii inaipa serikali ya Beijing nafasi ya kusema, Sisi kama serikali hatuhusiki, hiyo ni biashara ya kampuni binafsi. Hii inaifunga mikono Marekani kutoa adhabu ya moja kwa moja kwa serikali ya China.
Zamani, kupata picha za setilaiti zenye ubora wa juu ilikuwa ni siri ya majeshi makubwa tu. Leo, kuna makampuni mengi ya kibiashara yanayouza picha hizi kwa mtu yeyote mwenye pesa. Tukio hili la Jordan linaonyesha udhaifu mkubwa wa usalama wa dunia: Mataifa na makundi ya kigaidi sasa yanaweza kununua taarifa za kiintelijensia kwa njia halali za kibiashara na kuzitumia kufanya mashambulizi ya kigaidi au ya kijeshi kwa usahihi wa asilimia 100.
