Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Araghchi, anasema maafisa wa Marekani wanakuza vichwa vya habari vinavyohusiana na mafuta ili kutengeneza pesa na kumuweka Trump kwenye vita.
Sehemu ambayo inaweza kuthibitishwa ni hali inayoendelea karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz). Washington na baadhi ya wafanyabiashara wanataja takwimu za takriban mapipa milioni 8 kwa siku, huku baadhi ya ripoti zikifikia karibu mapipa milioni 16.
Ufuatiliaji wa satelaiti na meli za mafuta mara nyingi unakadiria mtiririko huo kuwa kati ya mapipa milioni 2 na 6 kwa siku.
Baadhi ya tofauti hizi zinaweza kuelezewa kwa meli kuzima mitambo yake ya mawasiliano na kuhamishia mafuta kwenye meli nyingine zikiwa baharini, lakini mbinu hizo hazifafanui pengo lote la takwimu hizo.
Kwa hivyo, mgogoro uliopo ni juu ya kiasi gani halisi cha mafuta ghafi kinachopita Hormuz, badala ya ushahidi unaoonyesha kuwa maafisa walipata faida binafsi kutokana na tofauti hiyo ya takwimu.
Kiwango cha mafuta kilichokuwa kikipita kabla ya vita kilikuwa takriban mapipa milioni 20 kwa siku, na viwango vya sasa bado viko chini ya hapo.
Madai ya kukuza takwimu kwenye taarifa ni jambo moja; lakini shutuma tofauti za uwepo wa mpango wa siri wa kujipatia faida zinasalia kuwa madai tu kutoka Tehran.
Bei ya mafuta duniani haipangwi tu na uzalishaji halisi, bali na hofu na matarajio ya wafanyabiashara (System 1 thinking). Washington inapotangaza takwimu kubwa au kuonyesha kuna tishio Hormuz, inatengeneza hofu (panic). Hofu hii inafanya bei ya mafuta ipande ghafla. Araghchi anachomaanisha hapa ni kwamba, kuna maafisa wa Marekani ambao wanacheza mchezo mchafu wa kutengeneza hofu kwenye vyombo vya habari, kisha wanatumia taarifa za ndani kununua au kuuza hisa za mafuta na kupiga faida kubwa.
Tofauti kati ya takwimu za Marekani (mapipa milioni 8 mpaka 16) na zile za satelaiti (mapipa milioni 2 mpaka 6) inaonyesha wazi kuwa Takwimu ni Silaha. Marekani inaweza kuwa inakuza namba hizi makusudi ili kuiaminisha dunia kuwa Iran inaingiza pesa nyingi sana kupitia soko jeusi la mafuta, na hivyo kuhalalisha kuwekewa vikwazo vizito zaidi au hata mashambulizi ya kijeshi.
Kitendo cha meli kuzima mitambo na kupakiza mafuta baharini ni uthibitisho wa jinsi vikwazo vya Marekani vilivyotengeneza soko kubwa la magendo. Iran imeunda mtandao mzima wa meli ambazo hazionekani kwenye rada ili kuendelea kuuza mafuta (hasa nchini China). Hii inafanya iwe ngumu sana kwa upande wowote kuwa na takwimu sahihi asilimia 100%, na hivyo kutoa mwanya wa kila nchi kupika takwimu zinazoipendelea.
Kwa ufupi, huu siyo tu mvutano wa kiasi gani cha mafuta kinapita baharini, bali ni vita ya kimkakati ya nani anaongoza simulizi (narrative) kwenye vyombo vya habari ili kudhibiti bei ya soko na kuhalalisha maamuzi ya kisiasa na kijeshi.
@Swahili Prime Media